MAPYA!! SIRI YA JOBE NA SARR KUKATA RASTA ZAO
Mastaa wawili wa Simba SC, Babacar Sarr na Pa Omary Jobe wamefiuchua sababu za kuwa na muonekano mpya kwa kukata Rasta na kubaki na nywele fupi.
Wachezaji hao ni maingizo ya dirisha dogo msimu huu, lakini kati yao Kiungo Mkabaji Sarr ambaye ni Msenegal ndiye aliyekuwa wa kwanza kutua kikosini na kufuatiwa na mshambuliaji Jobe.
Jobe ambaye ni raia wa Gambia, amecheza mechi tano hadi sasa na amefunga mabao mawili na asisti moja huku Sarry akifunga bao moja pekee.
Akizungumza kabal ya kuondoka jijini Dar es salaam kuelekea mjini Abidjan-Ivory Coast, Sarr alisema kunyoa rasta na kubaki na kipara hakuna maana kubwa sana, lakini huo ni uamuzi wake binafsi kutaka kubadilisha mwonekano na kuwa simpo.
“Nimetaka kuwa tofauti na sio jambo kubwa la kuwashangaza, kwani lazima mtu abadilike badilike kidogo, pia niko huru sana na huu mwonekano mpya,” alisema na kuongeza wameamua kubadilika kwa sababu kwa sasa ni maswahiba.
“Ilikuwa ni uamuzi wetu tu, tulifikiria kwenda saluni kujiweka sawa, tukaamua tuzinyoe kwa pamoja, hakuna ambaye ametushinikiza, ni uamuzi wetu binafsi,” alisema Jobe ambaye ni sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichoelekea Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Asec Mimosas.
Wawili hawa hawana historia ya kucheza pamoja kwenye timu yoyote zaidi ya Simba SC na huenda wakawa marafiki wakubwa kwani wamejenga uswahiba ndani ya muda mfupi.