KOCHA wa Yanga, Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake kwa mambo makubwa kwa CR Belouizdad kwani walikuwa bora uwanjani, na yeye mwenyewe kuweka rekodi mbili ya kupeleka robo fainali kwa mara ya kwanza tangu 1998 na sasa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Amesema alianza vibaya baada ya ya makundi watu waliwachukia na kutokuwa na furaha, wao lakini jana wamekuwa bora amewasamehe waliokuwa hawana furaha ndio mpira sasa wanaangalia mbele.
Baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria uliochezwa juzi uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Gamondi alisema kwenye mpira ukitengeneza nafasi unatakiwa kutumia lakini sio zote unaweza kutumia walichokifanya wachezaji wake ni kizuri.
Amesema kipindi cha kwanza tulitawala mchezo lakini wapinzani walikuwa wanajilinda ili wasifungwe mabao mengi, kipindi cha pili tulibadili mbinu na kuweza kupata mabao mengi.
“Tumeshafuzu bila kujali matokeo ya mechi iliyobaki lakini tunaenda kutafuta pointi ugenini dhidi ya Al Ahly, ninaifahamu vizuri Al Ahly, tutaenda kucheza kwa kufurahi bila ya presha.
Kwa kuwa tunahitaji alama katika mchezo huo ili tumalize kwa heshima tunaenda kufanyia kazi ubora na kusahihisha makosa yetu kwa ajili ya kutafuta heshima katika mchezo wetu wa mwisho,” amesema Gamindi.
Kiungo wa Yanga Mudathir Yahya, ameeleza kuwa siri kubwa ya uwezo wake wa kufumania nyavu ni kucheza nafasi ya Winga isiyoeleweka maana katika mechi zote alizofanikiwa kupata matokeo hachezi nafasi ya kiungo.
“Mnaweza kuona uwanjani nacheza kama kiungo lakini pia nakuwa winga kulingana na majukumu niliyopewa na benchi la ufundi, tumelipa kisasi na sasa tunaenda Misri kutembea huku tukihitaji kutafuta heshima,” amesema Mudathiri.
Kocha wa CR Belouizdad, Marcos Paquette amesema mashindano ni magumu kwao wamecheza na timu bora walijaribu kucheza vizuri lakini wamekutana na ugumu.
Ameongeza kukuwa pia joto lilikuwa kali kwa wachezaji wake walichoka haraka matokeo kwa kushindwa kufanya vizuri katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili na kuruhusu bao mbili za haraka haraka baada ya mapumziko.
“Matokeo ya Yanga kwa sasa yametukatisha tamaa lakini hawatachoka na wanaenda kupambana kujiandaa na mechi yao ya mwisho dhidi ya Medeama FC , tutatumia mchezo huu kuangalia makosa na kusahihisha kabla ya mechi yetu ya mwisho,” amesema Marcos.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, alikabidhi fedha kwa ajili ya “Bao la mama” ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kununua kila bao kwa timu za Taifa na klabu zinazoaakilisha nchini katika michuano ya kimataifa.
Mwana FA amesema kitendo cha Yanga kuingia hatua hiyo kwa mara ya kwanza, Tanzania kuiweka kwenye ramani na wanatamani kuona inafika mbali zaidi katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Naye Rais wa Yanga, Hersi Said amesema licha ya kuwaahidi wachezaji bonasi kubwa kabla ya mchezo walifanya mazungumzo na kudai watatumia falsafa waliyotumia Novemba 5, mwaka jana ili kuweza kumfunga CR Belouizdad bao 4-0 .
“Kulingana na kanuni lazima mchezo huu tushunde mabao 4-0 tulilazimika kuzungumza na wachezaji ili kuona jinsi gani ya kupata idadi hiyo, wakatoa ahadi kuwa aatatumia falsafa ya mechi ya Novemba 5, ili kusonga mbele katika mchezo wa leo na hilo limetimia,” amesema Hersi na kuahidi timu hiyo itaendelea kufanya vizuri katika hatua inayofuata.