MO DEWJI HASHIKIKI KWA UTAJIRI AFRIKA
Mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohammed Dewji ametajwa na Jarida la Forbes kuwa tajiri namba 12 barani Afrika na bilionea kijana zaidi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo.
Kwa mujibu wa jarida hilo Mo anayemiliki Kampuni ya Mohammed Enterprises Ltd (METL) amefanikiwa kupanda kiutajiri barani Afrika kutoka nafasi ya 15 hadi 12.
Utajiri wake umepanda kutoka Dola za Marekani 1.5 bilioni (Sh3.77 trilioni) mwaka uliopita hadi Dola 1.8 bilioni (Sh4.52 trilioni) jambo linalomfanya kuwa tajiri namba moja ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Orodha mpya ya Mabilionea wa Afrika:
1. Aliko Dangote: TZS trilioni 34.8
2. Johann Rupert and family: TZS trilioni 25.3
3. Nicky Oppenheimer & family: TZS trilioni 23.5.
4. Nassef Sawiris: TZS trilioni 21.8
5. Mike Adenuga: TZS trilioni 17.3
6. Abdulsamad Rabiu: TZS trilioni 14.7
7. Naguib Sawiris: TZS trilioni 9.5
8. Mohamed Mansour: TZS trilioni 8
9. Koos Bekker: TZS trilioni 6.7
10. Patrice Motsepe: TZS trilioni 6.7
11. Issad Rebrab & family: TZS trilioni 6.2
12. Mohammed Dewji: TZS trilioni 4.5