UHONDO unazidi kuwa mkali kwenye Kombe la Mtaifa ya Afrika AFCON kutokana na kuwa kila timu inaonyesha uwezo wake ndani ya dakika 90 ili kusaka ushindi.
Huku Miongoni mwa timu zilizoanza kwa ushindi katika mechi zao ni Mali ambapo kipa aliyeanza langoni ni Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja wa Yanga.
Katika mchezo uliochezwa jana Januari 16 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mali 2-0 Afrika Kusini. Mabao yalifungwa na Hamari Traore dakika ya 60 Lassine Sinayoko dakika ya 66.
Januari 17 ni mchezo wa kwanza kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itakuwa dhid ya Morocco saa 2:00 usiku, kwa taarifa Kamili kwenye kiungo hapo chini.
TAIFA STARS LEO DHIDI YA MOROCCO, WATAKE WASITAKE WAARABU WATAKAA TU!.