KAZI kubwa ambayo inapaswa kufanyika kuelekea kwenye mashindano ya kitaifa na kimataifa ni kufanya kweli kwa kila timu kupata matokeo mazuri.
Tumeona kwamba kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika, (AFCON) Tanzania ilikwama kutinga hatua ya 16 bora na kuishia kwenye hatua za makundi.
Kwa maana hiyo kuna makosa ambayo wachezaji waliyaona na kushindwa kuyatumia kwenye mechi zao na pia benchi la ufundi kuna makosa liliona yakashindwa kufanyiwa kazi kwenye mechi zilizofuata.
Mwisho ilishatokea kwamba Tanzania ilikuwa ni timu shiriki na matokeo yameigharimu kwa kushindwa kusonga mbele ni wakati wa kutazama wapi ambapo ilikuwa ni ngumu kuendelea katika hatua inayofuata.
Kila mmoja furaha yake ni kuona matokeo yanapatikana na kushindwa kupatikana kwa matokeo ni mwanzo wa kutafuta pale palipokuwa na makosa ili kazi ifanyikwe.
Yaliyotokea huwezi kuyabadili lakini yajayo kuna nafasi ya kujipanga upya na kuanza kufanya kazi kubwa kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata.
Kuna mashindano ambayo yataendelea kwenye ligi ambayo ni ya kitaifa na pia kuna timu ambazo zinashiriki mashindano ya kimataifa hapo ni muhimu kufanya kazi kubwa kupata matokeo mazuri.
Kushindwa kwenye mechi zilizopita sasa ni iwe mwanzo wa kupata ushindi kwenye mechi zijazo ambazo zitakuwa na ushindani mkubwa kila wakati.
Muda ni sasa na kila kitu kinawezekana ikiwa tu wachezaji wataamua na benchi la ufundi kuchanga karata zake kwa umakini, hivyo tu basi.