CHAMA AITISHA STARS “SISI TUTAWAFUNGA TU”
Mchezaji wa Simba SC na timu ya Taifa ya Zambia Clatous Chama amesema kwamba kwenye mchezo ujao ambao watakutana na Taifa Stats utakuwa ni mchezo mgumu ila wao kama Zambia watajitahidi washinde bila kujali lolote
“Kila timu bado ina nafasi ya kufuzu hatua inayofuata maana tumebakiwa na mechi mbili kila mmoja. Mechi itakuwa nzuri na ngumu kwasababu hata wao Tanzania wanataka kufuzu ila sisi tutapambana tuhakikishe tunashinda huo mchezo” amesema Chama
Stars mpaka sasa ikiwa haina point katika kundi F ambapo mpaka sasa imesalia na mechi mbili mchezo unaofuata ni dhidi ya Zambia.
Kulingana na kariba ya timu zote ambazo Stars imesaliwa na mechi ambazo inawezekana ikawa ndio mshindani halisi kutokana ni timu ambazo zinaendana kimazingira ambapo zinatokea, Hata kariba ya wachezaji na hata miundombinu.
Hivyo nafasi ya Stars kusonga mbele ni kuiombea kupata matokeo katika Mechi zake hizi mbili zilizosalia au kama ikipata ushindi dhidi ya Zambia na ikapata sare dhidi ya DR Congo basi hapo ni kuombea Morocco awatandike wote hawa wawili, ijapokuwa nafasi ya kusonga mbele kila timu bado inayo.