Meneja wa Mawasiliano na Habari timu ya Yanga SC, Ali Kamwe amesema kuwa wameamua kuondoa viingilio kwenye mechi yao na Mamelodi eneo la mzunguko ili kuwapa fursa mashabiki zao waingie kwa wingi
“Wote tunakubaliana mechi ya Mamelodi ni mechi kubwa zaidi kwenye robo fainali ya CAFCL msimu huu na Tunafahamu mechi itaisha usiku sana, kwa kuwajali mashabiki wetu na dhamira ya nchi yetu hasa kwenye sekta ya michezo Viongozi wetu wameamua jukwaa la 𝐌𝐙𝐔𝐍𝐆𝐔𝐊𝐎 litakuwa 𝐁𝐔𝐑𝐄” amesema Kamwe
“Viongozi wetu hawana tamaa ya fedha, ndio maana tumepunguza na kuondoa tiketi ya mzunguko kwa lengo la kuhakikisha wengi waje Uwanjani. Tumeweka maslahi ya mpira wa Tanzania mbele. Mechi ya Mamelodi ni kubwa mno lakini kwa kuwa lengo sio fedha ni hamasa basi tunawasihi mashabiki kujitokeza kwa wingi. Kiasi cha fedha ambacho ungelipia tiketi ya mzunguko basi utatumia kama nauli ya usafiri wa kukufikisha uwanjani na baada ya mchezo wetu uweze kurudi nyumbani salama” Alikamwe