KITAIFA

MASTAA YANGA WAPEWA KAZI HII NA KOCHA WAO

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hamdi Miloud ameweka wazi wachezaji wake wanafanya kazi kubwa kutafuta matokeo uwanjani jambo ambalo linapaswa kuwa endelevu kutokana na ushindani uliopo ndani ya ligi.

Miloud kibindoni ana tuzo ya kocha bora ndani ya Februari baada ya kukiongoza kikosi cha Yanga kwenye mechi 5 ambazo ni dakika 450 ushindi ilikuwa kwenye mechi nne sare moja ilikuwa JKT Tanzania 0-0 Yanga.

Katika mechi hizo tano safu ya ushambuliaji ya Yanga ilifunga mabao 16 na ukuta uliruhusu mabao mawili pekee kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.

Ni Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Yanga na Fred Minziro Kocha Mkuu wa Pamba hawa aliingia nao fainali na kuwashinda kwenye kuwania tuzo hiyo na mchezaji alichaguliwa kuwa Prince Dube ambaye anapewa mbinu na kocha huyo.

Miloud amesema kila mchezo ambao wanacheza una ushindani mkubwa jambo ambalo linawafanya wapambene kupata matokeo mazuri kila wanapoingia uwanjani.

“Ushindani ni mkubwa na wachezaji wanajituma kupata matokeo mazuri kwenye mechi ambazo tunacheza hivyo nina amini kwamba tutaendelea kuwa kwenye ushindani katika mechi zinazofuata.”

Yanga ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 58 baada ya mechi 22, safu ya ushambuliaji ya timu hiyo inayoongozwa na Dube na Clement Mzize wenye mabao 10 kila mmoja imetupia mabao 58.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button