KITAIFA

KAPOMBE AUKUBALI MZIKI WA TMA STARS, HAIKUWA KAZI RAHISI

SHOMARI Kapombe beki wa Simba amesema kuwa walikutana na ushindani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao TMA Stars katika mchezo wa hatua ya 32 bora CRDB Federation Cup uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.

Katika mchezo huo Machi 11 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 3-0 TMA Stars kwa mabao ya Valentin Nouma dakika ya 15, Sixtus Sabilo alijifunga dakika ya 19 na Leonel Ateba alifunga bao la tatu dakika ya 75.

Kwenye mchezo huo nyota Sabilo dakika ya 45 alifanya jaribio la hatari ambalo lilimpa tabu kipa namba mbili wa Simba, Ally Salim ambaye alikuwa langoni kwenye mchezo huo likiwa ni jaribio pekee lililokuwa na hatari zaidi kwa upande wa TMA Stars.

Shomari ameweka wazi kuwa waliingia kwa malengo yakupata ushindi kwenye mchezo huo jambo ambalo lilifanikiwa baada ya mchezo kukamilika.

“Ilikuwa ni mechi yenye ushindani mkubwa hasa ukizingatia kwamba hatua ya mtoano kila timu inatafuta ushindi, kushinda kwetu ni furaha na tunaamini kwamba tutaendelea kupambana kupata matokeo mazuri kwenye mechi zijazo.”

Simba inatinga hatua ya 16 bora inaungana na Yanga ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa KMC Complex Machi 12 2025.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button