KITAIFA
Lamine Yamal kuikoso Atletico Madrid kisa jeraha la Mguu.

Nyota wa klabu ya Barcelona na Timu ya taifa ya Hispania Lamine Yamal atakosekana kwenye mchezo wa nusu fainali wa kombe la mfalme (Copa Del Rey) siku ya kesho dhidi ya Atletico Madrid baada ya kupata jeraha la mguu kwenye mchezo uliopita wa laliga dhidi ya Las Palmas.
Lamine Yamal shows off painful-looking injury after Barcelona’s win over Las Palmas – Barca Blaugranes
Yamal alipata jeraha kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kuchezewa rafu mbaya na kutolewa nje dakika ya 85 ya mchezo huo ambao Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Taarifa kutoka Hispania zinaripoti kuwa kinda huyo ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake siku ya leo kutokana na jeraha hilo.