KITAIFA

EDO KUMWEMBE: BUSARA INABIDI ITUMIKE KWAAJILI YA TAIFA

EDO KUMWEMBE: BUSARA INABIDI ITUMIKE KWAAJILI YA TAIFA

“Unaweza kufika mbinguni umechoka kama unafuatilia uvumi wa mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize kwenda nje ya nchi. Pengine utasoma mengi kuhusu wachezaji wa Ligi Kuu ya Tanzania kutakiwa na timu za nje lakini jina la Mzize limezidi sasa.

Jana nimesikia kuna timu kutoka Ubelgiji imeweka mezani kiasi cha Sh2.5 bilioni za Kitanzania. Kabla ya hapo nimesikia mengi na umesikia mengi. Kwamba anatakiwa na Wydad Casablanca ya Morocco. Kwamba anatakiwa na TP Mazembe. Kwamba anatakiwa na Mamelodi Sundowns. Hizo ofa zote unazisoma kule Instragram. Na ofa hizo hizo unasikia kutoka kwa viongozi wa Yanga kwamba zipo mezani.

Binafsi sishangai kama Mzize anatakiwa. Ana umri mzuri katika pasipoti yake. Lakini zaidi ya kila kitu ni kwamba dunia kwa sasa ina uhaba wa washambuliaji. Hiki hiki ambacho unakidharau kwa Mzize elewa kwamba kuna washambuliaji wengi hawana. Hapa hapa nchini jaribu kujipa mfano wa uhaba wa washambuliaji. Namna ambavyo Yanga walimpoteza haraka Fiston Mayele baada ya kuikamata Afrika katika ufungaji. Wameteseka hasa. Waliwahi kumletea mshambuliaji mrefu kutoka Ghana, bwana Hafiz Konkoni lakini bado mambo hayakuweza kwenda sawa. Hata bwana Joseph Guede naye hakuweza.

Hata hivyo, inapofikia mchezaji anatakiwa na klabu fulani ambazo zinacheza katika ligi kubwa kuliko yetu nadhani busara inabidi itumike kwa ajili ya taifa. Labda mchezaji ataenda kupata uzoefu mkubwa zaidi kuliko alivyo sasa.

Iliwahi kutokea kwa Samatta, Simon Msuva na sasa inatokea kwa Novatus Dismas. Inaweza pia kutokea kwa Mzize kama akienda kucheza Ligi Kuu ya Morocco, au Afrika Kusini, ingawa itakuwa vema zaidi kama akienda Ubelgiji kama nilivyosikia.“

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button