GAMONDI AWASILISHA RIPOTI, VYUMA VITATU
ANGA leo usiku itakuwa Unguja, Zanzibar kwenye mechi ya Ligi kuwania usukani wa msimamo wa Ligi Kuu, lakini kocha wao Miguel Gamondi tayari ameshaanza hesabu za dirisha dogo la usajili.
Kuna hesabu kali zilizopo mezani kwake ambazo kama zikitimia huenda zikashangaza mashabiki ambao wanaamini kwamba timu hiyo tayari imetimia kwenye kila idara. Habari za ndani ambazo nimezipata ni kwamba sababu kubwa iliyomfanya Gamondi kurudi sokoni ni kutokana na malengo yake ya msimu huu lakini amechungulia ratiba ngumu ya ligi pamoja na mechi mfululizo vikamtisha.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema Gamondi amewasilisha ripoti yake ya awali akitaka kuongezwa kwa wachezaji watatu katika dirisha lijalo la usajili; Beki wa Kulia, Winga ya Kushoto na Mshambuliaji.