Meneja wa Havari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga, Ali Kamwe amefichua mipango ya klabu hiyo ambapo ameeleza kuwa Januari kutakuwa na ongezeko la mchezaji mwingine wa kigeni ndani ya kikosi hicho ambacho mpaka sasa tayari ni moto wa kuotea mbali.
“Nataka niwaambie tu Yanga hiç bado, Januari kutakuwa na ongezeko la mchezaji mwingine wa kigeni kwa hiyo haijakamilika tunahitaji kuchukua ubingwa wa Afrika” amesema Ali Kamwe.
“Huyo mchezaji aliyemsema Rais Hesi tumemleta alikuwepo uwanjani katika mchezo wa Dabi ya Kariakoo na amekuja kufanya mazungumzo na kusajili tayari kwa kuanza kazi katika michuano ya kimataifa” alisema Kamwe.
Inafahamika kuwa Yanga wanataria kuongeza baadhi ya wachezaji kwenye dirisha dogo, huku aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Fredy Michael akitajwa kutua kwenye kikosi cha Yanga .
Fredy amekuwa akionekana na wachezaji wa Yanga mara kadhaa, ikiwemo kambini na maeno mengine hali inayozidisha uwezekanao wa kuwa kwenye dirisha dogo huenda akatambulishwa mazima Jangwani.
Mbali na Fredy inafahamika kuwa Yanga iko kwenye mawindo ya kumpata kiungo fundi kutoka DR Congo ambapo jina lake na timu anayotokea likifichwa.
Hata hivyo Yanga wananafasi ya kusajili mpaka wachezaji 12 wa kigeni ambapo wengine watatumika kwa mashindano ya kimataifa.