TAARIFA kutoka ndani ya Yanga zinasema bado wanaendelea kupambania namna ya kuongeza mikataba ya nyota wake wawili, Pacome Zouzoua na beki Kouassi Yao.
Kwa Yao mambo yanaelezwa ni mepesi na huenda akawa wa kwanza kusaini mkataba, huku Pacome akiendelea kusikilizia kwani ndiye mchezaji ambaye tayari ana ofa tatu mezani kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Inataarifiwa kuwa Simba na Azam zimeandaa ofa nono ya kumshawishi kiungo huyo fundi kutoka Ivory Cost kujiunga nazo kwa lengo la kuongeza kikosi kwenye vikosi vyao.
Taarifa za ndani kabisa zinadai kuwa Simba haswa wamepania kumshusha Pacome wakiamini anaweza kuja kuziba pengo la Chama ambaye alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu.
Inasemekena kuwa Simba wameandaa zaidi ya dola za kimarekani 250,000 zaidi ya Tsh Milioni 500 kumshawishi ali ajiunge na miamba hiyo ya Msimbazi.
Simba wanamtaka Pacome kwa ajili ya kwenda kuimarisha eneo lao la mbele ambapo kumekosekana utulivu haswa kwenye kutengeneza nafasi za wazi.
Azam nao hawajabaki nyuma kwenye kumtaka kiungo huyo huku nao wakitenga ofa nono ya kumshawishi Pacome kwenda kutengenza pacha ya kazi na Fei Toto.