HIZI HAPA TAKWIMU ZA CHAMA KWENYE MECHI NNE ZA MWANZO, SIMBA WAMEJICHANGANYA
Kiungo wa Yanga, Clatous Chama ni yuleyule wa maamuzi magumu kwenye mechi ambazo anapewa nafasi ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Oktoba 22 2024 alifunga bao lake la kwanza kwenye ligi kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18 mbele ya JKT Tanzania na aitoa pasi moja dakika ya 23 kwa Pacome ambaye alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo.
Kumbuka kwamba bao la Chama dakika ya 43 ni Pacome alisababisha faulo kwa kipa Richard Dennis ambaye alijichanganya na kudaka mpira nje ya eneo lake la 18 akaonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja na mwamuzi wa kati Arajiga.
Kumbuka kwamba kwenye Kariakoo Dabi, Chama faulo aliyopiga dakika ya 86 ilibadili usomaji wa ubao na hata alipokuwa Simba faulo yake ya dakika ya 90 kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ilibadili usomaji wa ubao ikawa ni Simba 1-1 Azam FC
Hizi hapa takwimu za Chama kwa mechi nne za kwanza :-
Takwimu za kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Clatous Chama katika mechi nne za kwanza za msimu wa NBC Premier League 2024|25, ukilinganisha na mechi nne za kwanza kwenye misimu yake mitatu iliyopita.
Mechi nne za kwanza (2020|21)
◉ 4 – Games
◉ 2 – Goals scored
◉ 3 – Assists
◉ 5 – G/A
Mechi nne za kwanza (2022|23)
◉ 4 – Games
◉ 1 – Goals scored
◉ 1 – Assists
◉ 2 – G/A
Mechi nne za kwanza (2023|24)
◉ 4 – Games
◉ 2 – Goals scored
◉ 2 – Assists
◉ 4 – G/A
Mechi nne za kwanza (2024|25)
◎ 4 – Games
◎ 0 – Goals scored
◎ 0 – Assists
◎ 0 – G/A.