Baada ya jana usiku kufunga mabao matatu kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Raphinha amekuwa tishio kwasasa kuelekea mechi kubwa zaidi ya Ligi kuu Hispania dhidi ya Real Madrid ‘El Clasico’.
Raphinha hadi sasa msimu huu amecheza michezo 13 na kufunga mabao 9 zikiwemo ‘hat-trick’ 3 na asisti 8 hali inayomfanya kuwa mmoja wa wachezaji wakuchungwa zaidi kuelekea El Clasico.
Kwenye mchezo wa jana Barca iliichapa Bayern 4-1.