Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 inashuka dimbani leo dhidi ya Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) Kanda ya CECAFA.
Mchezo huo utafanyika kwenye uwanja wa KMC uliopo, Mwenge, Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam.
Katika nusu fainali ya pili Kenya itachuana na Burundi kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.
Tanzania imeshika nafasi ya pili nyuma ya Kenya katika kundi A lililokuwa na timu tano zikiwemo Rwanda, Djibouti na Sudan.
Uganda iliongoza kundi B lililokuwa na timu 4 ikifuatiwa na Burundi ambapo timu nyingine ni Sudan Kusini na Ethiopia.