KUELEKEA ‘DABI’ …KWA REKODI HIZI ZA FADLU..YANGA WATATOBOA KWELI.?
Kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ni mechi tano kimeshuka uwanjani ndani ya Ligi Kuu Bara ambazo ni dakika 450.
Katika mechi hizo ushindi mechi nne Simba ilipata kwa kukomba pointi tatu mazima ambazo ni 12 ndani ya uwanja na iliambulia sare mchezo mmoja.
Ikumbukwe kwamba kwenye sare hiyo ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union waligawana dakika 45 za kazi ambapo kipindi cha kwanza ilikuwa mali ya Simba ilipofunga mabao mawili na kipindi cha pili Coastal Union walifanya kweli kwa kufunga mabao mawili.
Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC, Mwenge Simba walikuwa nyumbani katika mchezo huo ikiwa ni mara ya kwanza kwa kipa Mussa Camara kutunguliwa mabao hayo kwenye mechi za ushindani.
HIZI HAPA MECHI ZA USHINDI
Simba 3-0 Tabora United Simba 4-0 Fountain Gate Azam FC 0-2 Simba Dodoma Jiji 0-1 Simba.
Safu ya ushambuliaji imefunga mabao 12 na ukuta umeruhusu mabao 2 ndani ya dakika 450 msimu wa 2024/25 kwenye msimamo ipo nafasi ya 2 ikiwa na pointi 13 na vinara ni Singida Black Stars wakiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita.
Kituo kinachofuata ni Kariakoo Dabi mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa Oktoba 19 2024.