DIARRA KIPA WA YANGA AJENGA UFALME WAKE
KWENYE eneo la makipa Bongo Djigui Diarra wa Yanga ameendeleza kujenga ufalme wake akiwa amecheza jumla ya mechi 8 za ushindani bila kufungwa ndani ya uwanja.
Mechi hizo ambazo amcheza ni dakika 720 kwa Diarra amekomba akiwa uwanjani katika mechi za ushindani msimu wa 2024/25 akishirikiana na wachezaji wengine wa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Moja ya mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa kwake ni ule dhidi ya Ken Gold uliochezwa Uwanja wa Sokoine ambapo katika dakika za jioni mastaa wa Ken Gold walifunguka na kuanza kushambulia kwa kasi huku ule dhidi ya KMC mbinu kubwa ya wapinzani ilikuwa kujilinda.
Ni mechi nne katika Ligi ya Mabingwa Afrika ameanza langoni kuanzia hatua ya awali, hatua ya pili ambapo Yanga kwa sasa imetinga hatua ya makundi na imepangwa Kundi A mchezo wake wa kwanza itakuwa dhidi ya Al Hilal unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Dakika nyingine 360 ilikuwa kwenye mechi nne za ligi ambapo mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga na mabao yakifungwa na Maxi Nzengeli na Clement Mzize.
Kituo kinachofuata kwa Yanga ni Kariakoo Dabi dhidi ya Simba unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 ambapo timu zote hesabu ni kupata pointi tatu.