KITAIFA

YANGA WAREJEA KAMBINI KUWAHI SIMBA

Kikosi cha timu ya Yanga SC kimerudi katika kambi yao ya Avic Town kujiandaa na mchezo wao wa NBC Premium league dhidi ya Simba SC, Oktoba 19.

Yanga SC walitoa mapumziko ya siku kadhaa baada ya kumalizika kwa mchezo wao na Pamba Jiji na kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Meneja Mkuu wa timu hiyo Walter Harrison amesema wachezaji wao ambao hawako katika majukumu ya timu za taifa wanaendelea na maandalizi ya mchezo huo.

“ Timu imesharudi kambini kujiandaa na mchezo huo ambao tunaamini tunaenda kuwapa furaha mashabiki wetu.

“ Timu itaendelea na mazoezi hadi Jumamosi na Jumapili itakuwa mapumziko. Tunafanya hivi ili wachezaji wengine walioko katika timu za taifa wakirudi kambini wawe sawa kiutimamu na hawa waliobakia kambini “ alisema Walter.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button