MAKUNDI YA KLABU BINGWA AFRICA 2024/2025 (CAF CHAMPIONS LEAGUE GROUPS)
Makundi ya Klabu Bingwa Africa 2024/2025 | Makundi ya Caf Champions League 2024/25 | Kundi la Yanga CAF Klabu Bingwa Afrika 2024/2025
Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, limetangaza makundi ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) kwa msimu wa 2024/2025. Hafla hiyo iliyosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka barani kote, imefanyika jijini Cairo, Misri, ambapo vilabu bora vya Afrika vilivyofuhu hatua ya makundi vilipangwa katika makundi rasmi ya michuano hii mikubwa ya vilabu barani.
Msimu huu, mashindano ya Klabu Bingwa Afrika yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku timu zinazoshiriki zikiwa na rekodi nzuri katika soka la kimataifa. Kila kundi limeleta changamoto za kipekee, na mashabiki wanaweza kujiandaa kwa mechi zenye mvuto na ushindani mkubwa zitakazowakutanisha mabingwa wa zamani na timu zinazoibuka kwa kasi.
Baada ya droo hii, wachambuzi wa soka wameanza kutoa maoni yao kuhusu makundi, huku wengi wakitabiri kuwa Kundi A litakuwa “kundi la kifo” kutokana na uwepo wa timu ambazo zipo katika kiwango bora kama Yanga sc, Tp Mazembe na Al Hilal SC. Hata hivyo, michuano hii imekuwa na misukosuko mingi hapo awali, na hakuna anayeweza kutabiri kwa uhakika ni timu gani itaibuka kidedea
Makundi ya Klabu Bingwa Africa 2024/2025 (Caf Champions League Groups)
Kundi A:
- TP Mazembe (DR Congo)
- Yanga (Tanzania)
- Al Hilal SC (Sudan)
- MC Alger (Algeria)
Kundi B:
- Mamelodi Sundowns (South Africa)
- Raja Club Athletic (Morocco)
- AS FAR (Morocco)
- AS Maniema Union (DR Congo)
Kundi C:
- Al Ahly SC (Egypt)
- CR Belouizdad (Algeria)
- Orlando Pirates (South Africa)
- Stade d’Abidjan (Ivory Coast)
Kundi D:
- ES Tunis (Tunisia)
- Pyramids FC (Egypt)
- GD Sagrada Esperance (Angola)
- Djoliba AC (Mali)
Je, unadhani ni timu gani zitafuzu kutoka katika kila kundi? Tuandikie maoni yako hapa chini!