KIMATAIFATETESI ZA USAJILI

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU TAREHE 07.10.2024

Real Madrid huenda wakamnunua Trent Alexander-Arnold Januari, Liverpool wanataka kuongeza mikataba miwili, na Paul Pogba yuko tayari kuanza upya nje ya Juventus.

Real Madrid walikuwa na mpango wa kumsajili beki wa Uingereza Trent Alexander-Arnold, 25, kwa uhamisho wa bure msimu ujao wakati mkataba wake na Liverpool utakapokamilika, lakini huenda wakamnunua mwezi Januari baada ya beki wa Uhispania Dani Carvajal, 32, kupata jeraha baya la goti. (Sport – kwa Kihispania)

Liverpool wanaendelea na mazungumzo ya kandarasi ya mabeki wawili muhimu – Jarell Quansah, 21, na beki wa Ufaransa Ibrahima Konate, 25. (Mirror)

Paul Pogba, 31, anajadiliana na Juventus kwa lengo la kumaliza msimu wake wa pili na klabu hiyo ya Serie A na kuanza upya baada ya marufuku yake ya kutumia dawa za kusisimua misuli kupunguzwa na Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo. (Mail)

Wolves hawana nia ya kumtimua meneja Gary O’Neil lakini watampa muda wa kubadilisha kikosi chake baada ya kushindwa mara sita katika mechi saba za mwanzo za Ligi Kuu ya Uingereza. (Telegraph)

Manchester City wametenga pauni milioni 80 kwa usajili wa wachezaji katika dirisha la usajili la Januari baada ya Rodri ya kujeruhiwa. (Football Insider)

West Ham wana nia ya kumrejesha mshambuliaji wa zamani wa Leicester na Newcastle Ayoze Perez kwenye Ligi ya Premia kwa matumaini kwamba mchezaji huyo wa Villarreal mwenye umri wa miaka 31 anaweza kuboresha safu zao za mashambulizi. (Caught Offside)

Kocha wa zamani wa Barcelona Xavi ​​anapigiwa upatu kuongoza mradi wa kujenga upya kikosi cha Old Trafford iwapo Erik ten Hag ataondoka Manchester United. (El Nacional – kwa Kihispania)

Jaribio la Newcastle United kumsajili mshambuliaji wa Lille Jonathan David, 24, limepata pigo baada ya Barcelona kuingia katika zabuni. (Shields Gazette)

Liverpool wameungana na Newcastle na Tottenham katika mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji Eberechi Eze, 26, kutoka Crystal Palace. (Football Insider)

Barcelona wanamfuatilia winga wa Bayern Munich Leroy Sane, 28, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sport – kwa Kihispania)

Klabu za Ligi Kuu ya England ikiwemo Arsenal, Wolves, Everton na Chelsea zimekuwa zikimfuatilia beki wa Santos mwenye umri wa miaka 18 kutoka Brazil Joao Pedro Chermont. (Caught Offside)

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button