Beki wa Taifa Stars, Dickson Job aliumia dakika ya tisa ya mchezo wa Taifa Stars baada ya kugongana na kiungo wa Guinea na kulazimika kutolewa dakika ya 11 nafasi yake ikichukuliwa na Bakari Mwamnyeto. Akizungumza jana, Job alisema baada ya kukutana na ajalih iyo ndani ya uwanja wakati anatolewa alipata wasiwasi kama hataweza kuona tena kufuatia kushindwa kuona kitu kwa takribani dakika moja.
Job alisema hakuwa anaona kitu mbele hali iliyomshtua ambapo bado hafahamu aligongwa na kitu gani kwenye kichwa chake kiasi cha kupoteza netiweki hadi alipopatiwa huduma ya kwanza
“Sikuwa naona kitu, kuna rangi ambazo hadi sasa sizitambui zilikuwa zinanijia mbele halafu ilikuwa kama dakika hivi sielewi kitu gani nakiona mbele, kiukweli ilinitisha sana,” alisema Job. Hata hivyo, Job alisema baada ya matibabu alipo-tolewa hali yake ilianza kuimarika na macho yake kurudi kwenye ufanisi wake.
“Nipo sawa sasa naona vizuri, mashabiki wasiwe na wasiwasi nitarudi kazini kwenye majukumu yangu, hadi sasa ninavyojisikia naona nitaweza kuwa sehemu ya timu yangu ya Yanga kwenye mechi inayofuata kule Addis Ababa.”