Mchezaji wa Asernal aliyejiunga kwa mkopo kwenye klabu hiyo akitokea Chelsea Raheem Sterling Muingereza mwenye asili ya Jamaica amebatizwa na kubadilisha imani yake katika Dini ya Kikisto.
Baadhi ya video zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Sterling akiwa na mavazi meupe akibatizwa huko nyumbani kwao nchini Jamaica alipozaliwa.
Sterling amesema amefanya uamuzi huo baada ya kugundua kuwaalikuwa akikosa furaha kwa kuishi maisha ya kujionyesha lakini moyoni hakutaka kuiacha njia aliyokuzwa nayo na mama yake ya kumuamini Mungu na kuwa mtu wa ibada, anasema sasa ametambua nini anapaswa kufanya yeye binafsi na hapo awali aliongozwa na Ego na sio Upendo wake kwa Mungu ila sasa ameamua kuchukuwa njia sahihi.
Raheem anasema amehamasishwa na mama yake mzazi ambae alikuwa ni mtu wa maombi muda wote na imani kubwa aliyokuwa kwa Mungu.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 ambaye amewahi kuitumikia Timu ya Taifa ya Uingereza ni miongoni mwa wachezaji wachache waliofanikiwa kuvitumikia vilabu vikubwa vya Uingereza kama Liverpool,Man City, Chelsea na sasa akiitumikia Arsenal.
Mwamba amerudi kuaga nyumbani mjipange.