Klabu ya Manchester City imepata pigo baada ya beki wao wa kati Nathan Ake kuumia akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uholanzi inayoshiriki michezo ya UEFA National League.
Ake aliumia msuli wa paja na kushindwa kuendelea na mchezo dakika ya 45 kwenye mechi ya UEFA National League dhidi ya Ujerumani uliochezwa jana nchini Uholanzi na kumalizika kwa sare ya 2-2 kwenye dimba la Johan Cruyff Arena.