KITAIFA
RASMI: AZAM YAACHANA NA KOCHA DABO
Baada ya mfululizo wa matokeo mabaya kwenye ligi kuu Tanzania bara na michezo ya kuwani kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya Mabingwa Afrika, klabu ya Azam leo septemba imefikia makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba na aliyekuwa kocha wao mkuu Youssuph Dabo raia wa Senegal.
Daboi ambaye amehudumu Azam kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee ataondoka na wasaidizi wa benchi lake la ufundi aliokuja nao Tanzania.
Kwa kipindi hicho Azam wakisaka kocha wa kurithi mikoba ya Dabo kikosi hicho kitakuwa chini ya makocha wa timu za vijana.