NYOTA wa kimataifa ndani ya Yanga, Khalid Aucho anaingia kwenye orodha ya namba sita watembeza mikato ya kimyakimya ndani ya uwanja kutokana na kuwa kwenye mwendelezo wa kasi hiyo katika mechi za hivi karibuni.
Ipo wazi kwamba Aucho ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Miguel Gamondi amekuwa na mwendelezo wa matukio ya kutembeza mikato ya kimyakimya jambo ambalo liliwahi kumsababishia adhabu ya kufungiwa mechi tatu msimu wa 2023/24.
Kutokana na mwendo huo anapaswa kubadilika kàtika mikato yake ya kimyakimya kutokana na kuwaumiza wachezaji wenzake.
Ikumbukwe kwamba katika Kariakoo Dabi alimpeleka nje ya uwanja mtembeza mikato ya Simba Sadio Kanoute.
Kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alimchezea faulo Ibrahim Ajibu na kàtika mchezo dhidi ya KMC Awesu Awesu alipata tabu kinomanoma.
Ilikuwa ni Februari 17 Aucho alicheza zaidi ya faulo tatu kwa nyota Awesu na alionyeshwa kadi moja ya njano ikiwa ni kadi ya kwanza kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Yanga ilishinda kwa mabao 3-0.
Ana balaa kiungo Khalid Aucho kwenye mikato ya kimyakimya ndani ya uwanja kwa kuwa ni namba sita mkabaji. Muhimu kuongeza umakini.