KITAIFA

FEI TOTO AMFUATA ENG HERSI, AMKUMBATIA HADHARANI

MUDA ambao timu ya Azam FC inakwenda kuchukua medali ya mshindi wa pili wa michuano ya Ngao ya Jamii, kama kuna tukio kilikuwa linasubiriwa basi ni kiungo Feisal Salum Fei Toto kuonana uso kwa uso na Rais wa Yanga injinia Hersi Said na wamekutana bana.

Katika zoezi hilo la kupokea medali Fei Toto amekutana na Hersi ambaye alikuwa jukwaa la viongozi walioshiriki kutoa zawadi ambapo  kwa mara ya kwanza wakakutana.

Hata hivyo, Fei Toto hakuwa na shida na mtu, akasalimiana na Hersi kwa kupeana mikono kisha wawili hao kukumbatiana na kuongea kwa sekunde chache.

Wakati wakisalimiana na kukumbatiana mashabiki wa Yanga wakalipuka kwa furaha wakishangilia  kwa nguvu, huku Fei akiondoka na medali akiwa ameivaa kisha kuivua baada ya mwendo mfupi.

Awali Feisal wakati anaondoka Yanga aliwahi kukaririwa akisema hata rejea timu hiyo endapo Hersi atakuwa Rais wa klabu hiyo.

Tangu ameondoka Yanga Feisal ameshawafunga waajiri wake wa zamani mabao matatu kwenye mechi tofauti za mashindano.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button