LICHA ya kikosi cha Simba kugotea nafasi ya tatu kwenye Ngao ya Jamii na washambuliaji wake kufunga bao moja ndani a dakika 180 uongozi wa Simba umebainisha kuwa bado kuna kitu ambacho kipo kwenye timu hiyo.
Simba imegotea nafasi ya tatu kwenye Ngao ya Jamii huku bingwa akiwa ni Yanga iliyopata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Azam FC na Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameandika namna hii kwenye ukurasa wake wa Instagram: “Nimewatazama wapinzani wote msimu huu naiona Simba yetu ikifanya maajabu ya dunia
“Mpaka sasa Simba ndio timu yenye wachezaji bora wenye viwango vikubwa mno, kilichobaki ni Mwalimu kutengeneza timu yenye mtiririko, muunganiko na maelewano ya pamoja.
“Eneo pekee linalohotaji nguvu mpya ya nje ni eneo la ushambuliaji nalo viongozi wetu wanakamilisha mpango hivi punde. WanaSimba tuwe na subira tumpe nafasi mwalimu wa kufanya kazi yake tutakapoanza kula matunda ya furaha kila mtu atapata tunda lake.
“Ubaya Ubwela unaenda kukamilika.”