Inawezekana naona tofauti na wengi lakini naona kuwa lazima kuna mambo kadhaa ambayo Simba wanapaswa kubadilisha katika kikosi chao ili kukifanya kuwa bora…
Mechi iliyopita Vs JKT kunaweza kuwa na sababu ya kiwanja lakini unaona suala la kikosi kinachopambana linabaki kwa baadhi ya wachezaji na wengine wanaonekana kuwa slow au kama wamechoka hivi…
Kuna vitu vinabadilika lakini yanapaswa kuwa mabadiliko ya pamoja na kwa kuwa Simba sasa inarejea kimataifa na fainali yao ni Vs Asec ugenini, lazima FIGHTING SPIRIT iwe ya KIWANGO CHA JUU ili kupata majibu sahihi.
Uwezo bila juhudi na maarifa navyo vinaweza visiwe na faida….UKITULIA…UTANIELEWA…
Mchezo ujao kwa Simba kimataifa unatarajiwa kuchezwa Februari 23 ambao utakuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tayari kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas.