KITAIFA
MWANASHERIA SIMBA AZUNGUMZA UKWELI KUHUSU AWESU NA MASHAKA
MWANASHERIA wa Simba, Hosea Chamba amesema wanasubiri hukumu kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji juu ya wachezaji Awesu Awesu na Valentino Mashaka.
.
Nyota hao waliosajiliwa hivi karibuni mashauri yao yalisikilizwa jana katika ofisi za TFF, kutokana na klabu za Geita Gold na KMC kuishtaki Simba.
.
“Awesu na Mashaka sisi tumewasajili wakiwa wachezaji huru hivyo uwepo wa kesi kutoka timu hizo mbili tunasubiri hatma zake kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji,” amesema Hosea Chamba.