Katika mkutano wa waandishi wa habari ambao ulifanyika leo, Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Kocha Mkuu wa Yanga, Gamondi alikumbushiwa matokeo ya Ngao ya Jamii msimu uliopita na kusema hayana nafasi kwake maana huu ni mchezo mpya.
“Mechi zilizopita kwangu hazina nafasi kuelekea mchezo ujao kwa sababu huu ni mchezo mpya, hatujui sana kuhusu Simba, jambo muhimu ilikuwa ni sisi kujiandaa na sio kuwafuatilia,naweza kusema tumefanya hilo kwa zaidi ya asilimia 75,” Gamondi amesema na kuongeza;
“Tupo tayari kwa ajili ya kukabiliana nao,siku zote nimekuwa nikitoa heshima kwa wapinzani wangu, najua kuwa Simba inawachezaji wapya na benchi jipya la ufundi hivyo watakuwa hali mpya kwa hiyo itakuwa mechi ngumu sana na naweza kuiweka katika mzani wa 50/50.
“Kikawaida ni ngumu kujua nini kinaweza kutokea, kesho ni mchezo wa mashindano hivyo utawakuwa mchezo mgumu, naamini utakuwa mchezo mzuri na wa ushindani lakini mpango wangu ni kupata ushindi kwenye mchezo huo, ni kweli kwamba kwenye mchezo uliopita (dhidi ya Red Arrow) tulipoteza sana nafasi hivyo tumekuwa kazi ya kufanya msahihisho.” Amesema Miguel Gamondi.
Simba na Ynaga kesho zitacheza mchezo wa Nusu fainali ya kombe la Ngao ya Jamii, katika uwanja wa Mkapa majira ya saa1:00 usiku.