KIMATAIFA
KAMA MASIHARA HIVI LAKINI NDIO ANASEPA
Taarifa zinaeleza kuwa Atletico Madrid na Manchester City zinakaribia kufikia makubaliano ya kuuziana Julian Alvarez raia wa Argentina kwa dau la pauni million 75.
Wakurugenzi wa timu zote mbili Gil Marín wa Atletico Madrid na Ferran Soriano wa Manchester City wamefanya mazungumzo usiku wa kuamkia leo.
Endapo Dili hilo litakamilika basi Atletico Madrid watakuwa tayari kumuuza mshambuliaji wao Samu Omorodión anawindwa na Chelsea.