SIMBA YATAMBIA MASHINE ZAO ZA KAZI 2024/2025
AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wachezaji wote waliopo ndani ya kikosi cha Simba wapo tayari kupambania uzi wa Unyamani kuwapa furaha Wanasimba.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Simba iligotea nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya mechi 30 ikiwa na pointi 69 itapeperusha bendera ya Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na Coastal Union ya Tanga iliyogotea nafasi ya nne.
Yanga ambao ni mabingwa wa ligi na Azam FC iliyogotea nafasi ya pili hizi itakuwa kwenye anga la kimataifa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Miongoni mwa wachezaji waliopo ndani ya Simba ni Deborah Fernandez, Edwin Balua, Mzamiru Yassin, Mhamed Hussein, Ayoub Lakred, Camara Mousa, Kibu Dennis.
“Wachezaji wote wa Simba wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25 na tunatambua kwamba msimu uliopita haukuwa mzuri kwetu kutokana na kushindwa kufikia malengo yetu lakini tunaanza upya kuyakimbiza malengo yetu hilo inawezekana.’
Agosti 8 2024 ni Kariakoo Dabi, Simba v Yanga katika Ngao ya Jamii, Uwanja wa Mkapa na Coastal Union itacheza dhidi ya Azam FC, Uwanja wa New Amaan Complex fainali itachezwa Uwanja wa Mkapa.