HISTORIA YA KOCHA WA SIMBA FADLU DAVIS, MAMBO MAZURI YAJA
FADLURAGHMAN DAVIS alizaliwa Mei 21 mwaka 1981 pale Cape Town mji uliopo kusini magharibi mwa taifa la Afrika Kusini, alizaliwa kufunga magoli na kueneza mabalaa yake, alizaliwa kwaajili ya watu wa mpira kumaliza hamu zao na kutazama kile alichozaliwa nacho.
Watu wa Martzburg United walianza kumfaidi zaidi uwanjani kabla hajawa kocha msaidizi na baadae kocha mkuu ambapo anakumbukuwa zaidi kwa uwezo mkubwa aliouonyesha kwa kukuza makinda bora na kuendeleza chembe chembe za hulka yake ya kuweka mpira nyavuni kwa makinda wengine wanaochipukia.
Akiwa kama kocha msaidizi msimu wa 2019/20 ndani ya Orlando Pirates alifanikiwa kuunda muundo mwingine uliosaidia kupata vijana bora kutoka vikosi vya academy kisha kwenda senior team na kufanya mabalaa makubwa huko, ndani ya SIMBA SC wachezaji wadogo kama Edwin Balua, hama Ladack Chasambi hukuwafaidi sana msimu uliopita watazame msimu huu
Pale Orlando Pirates yupo Bandile Shandu mchezaji kipenzi ambaye maisha yake katumikia Martizburg College na Orlando Pirates pekee, achana na Siphesihle Ndlovu mtaalamu mwingine alitengenezwa na Fadlu Davies kutoka timu za vijana mpaka Mabakhabhaka Yeses, tuseme R.I.P Mlondi Dlamini fundi ambaye kwenye umri wa miaka 20 tu alibebewa mabango
FADLURAGHMAN DAVIS, Kabla hajatua Raja Casablanca ya nchini Morroco ambapo msimu uliopita 2023/2024 alinyanyua ubingwa wa Botola mikononi mwake akiwa kocha msaidizi pasipo kupoteza mchezo wowote!! Alianza kusaidia kwanza kwenye timu za Russia kabla ya Raja Casablanca na sasa ni zamu ya SIMBA SC kufurahi kwa pamoja
Mechi ya jana, kaanza na mkongwe Fabrice Ngoma kama holding mmoja kando ya mtu mzima Mzamiru Yassin na mtoto mmoja wa Ali Awesu katikati ya dimba timu ikashawishi kwa soka lenye radha inakokufanya usubiri kungoja kipindi cha pili kusubiri Jean Charles Ahoua hama Joshua Mutale wangerudi vipi?!! Baada ya mabadiliko half time kila mmoja alitazama shughuli kubwa iliyofanyika kule Ismailia, mbali kabisa na Tanzania kocha Fadlu Davis anakuonyesha nini kinakuja siku zijazo.