Klabu ya Soka ya Young Africans ya Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa timu bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati.
Ubora wa klabu hiyo unatokana na uongozi imara wa Eng Hersi Said na kamati yake ya Utendaji, lakini pia namna wanavyofanya mambo yao kisomi na kisasa zaidi.
Hersi amekuja na mtazamo tofauti katika kuiendesha Young Africans jambo ambalo linazifanya klabu zingine kuiga kile anachokifanya, lazima tukiri kwamba Hersi ana akili nyingi, wakati huohuo ana mikakati thabiti ya kuifanya Football tofauti na watu wanavyomfikiria.
Hersi kwa sasa ni Rais wa Umoja wa Vilabu barani Afrika na anakua Rais wa kwanza Mtanzania na anakua Rais wa kwanza tangu kuanzishwa kwa Umoja huo. Itoshe kuamini kwamba kwa aina ya viongozi wa soka tulionao katika taifa letu, Hersi amejipambanua na ninamuona akiwa na uwezo wa kipekee.
Kutokana na namna anavyoenda, binafsi namuona Eng Hers Said akiwa Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika kwa miaka ijayo kwakua akili ya kuendesha mpira wa kimapinduzi anayo lakini pia fedha anayo. Kikubwa Tumuombee aweze kutimiza azma yake ya kuwa Rais wa CAF kutoka Tanzania.
Kama nchi tumekuwa tukikosa viongozi wa kujipenyeza kuzitafuta fursa jambo ambalo Hersi analifanya bila woga wowote na wote tumeona mafanikio yake.