Mtambo wa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara na Yanga , Aziz KI hajawa kwenye kikosi hicho katika mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 270 huku majukumu yake ya mapigo huru yakiwa kwenye miguu ya Pacome Zouzoa ambaye alikuwa na balaa.
Sababu kubwa ya Aziz mwenye mabao 10 na pasi mbili za mabao kutokuwa kwenye mechi hizo alikuwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Burkina Faso ambayo ilikuwa inashiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, (AFCON).
Mchezo wa mwisho kwa Burkina Faso ilikuwa dhidi ya Mali iliyoishia hatua ya robo fainali langoni alianza kipa Djigui Diarra ambaye naye anacheza ndani ya Yanga.
Ni mchezo wa raundi ya pili Azam Sports Federation ilikuwa dhidi ya Hausing FC, Uwanja wa Azam Complex Yanga iliposhinda kwa mabao 5-1 kisha kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar 0-0 Yanga ilikuwa ni ligi na dakika 270 zilikamilika Yanga 1-0 Dodoma Jiji.
Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Pacome alipiga faulo dakika ya 56, 82,90 na alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 69. Mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Pacome alipiga kona dakika ya 60 na alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 60.
Hivyo mikoba ya Aziz KI ilikuwa kwenye miguu ya Pacome ambaye alikuwa akishirikiana na wachezaji wengine wa Yanga kutimiza majukumu yao ya kila siku uwanjani.
Katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons tayari KI alirejea lakini alianzia benchi kwenye mchezo huo Pacome alifunga na kutoa pasi moja ya bao ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba uliposoma Prisons 1-2 Yanga.