KIMATAIFA

MFAHAMU MCHEZAJI MPYA WA ARSENAL

Wakati klabu ya Bologna ilipotangaza kuwasili kwa Riccardo Calafiori kutoka FC Basel mwishoni mwa Agosti mwaka jana, saa chache tu kabla ya kumalizika kwa dirisha la uhamiaji la wachezaji soko wachache sana walikisia jinsi hatua hiyo ingefanikiwa.

Kufuatia kuwasili kwa Jose Mourinho huko Roma mwaka 2021, jiji la nyumbani la Calafiori na klabu aliyokulia, nafasi na wakati wa kucheza vilikuwa adimu kwa beki huyo.

Hilo lilimtia moyo kukubali uhamisho wa kudumu kwenda kwa wababe wa Uswizi Basel katika msimu wa 2022.

Licha ya kuwa mara kwa mara katika timu za vijana za Italia, Calafiori alianza kuteleza kutoka kwenye rada ya soka ya Ulaya kabla ya mkurugenzi wa kiufundi wa Bologna Giovanni Sartori alipomnyatia.

Ilimchukua miezi 11 kabla msimu wa kwanza kamili wa Calafiori katika ligi ya Serie A kulimalizika kwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa, kabla ya kuthibitishwa kuwa mchezaji bora wa Italia kwenye Euro 2024 na thamani yake sokoni kuongezeka mara 12.

Sio wachezaji wengi kote barani Ulaya wanaweza kudai ongezeko kama hilo ndani ya kipindi kifupi kama hicho – na imemfanya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kuhamia Arsenal kwa ada ya hadi £42m ikiwa ni pamoja na nyongeza.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button