KIMATAIFATETESI ZA USAJILI

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE 30-07-2024

Arsenal wanavutiwa na mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen, klabu hiyo ya Italia huenda ikamuuza Osimhen kwa Chelsea kama sehemu ya mpango wa kubadilishana na Romelu Lukaku, na Everton wanakaribia kumsajili beki wa Lyon Jake O’Brien.

Arsenal bado wanamtaka mshambuliaji wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen, 25. (Corriere dello Sport – kwa Kiitaliano)

Napoli pia wanavutiwa na mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, na huenda wakamjumuisha katika mkataba wa kubadilishana na Osimhen. (Guardian)

Mlinzi wa Jamhuri ya Ireland Jake O’Brien, 23, amewasili Merseyside kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya uhamisho wake wa pauni milioni 17 kutoka Lyon kwenda Everton. (Guardian)

Everton huenda wakawasilisha ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Strasbourg na Senegal Habib Diarra, 20. (L’Equipe – kwa Kifaransa)

Vilabu kadhaa kutoka Ligi ya England na nje ya nchi vinawania kumsajili winga wa Luton Mholanzi Tahith Chong, 24, kwa takriban £10m. (Sky Germany)

West Ham wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Ufaransa na Monaco Youssouf Fofana, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anavutiwa na klabu ya AC Milan. (Givemesport)

Kipa wa zamani wa Manchester United David de Gea, 33, hatajiunga na Genoa, na Mhispania huyo hakuwahi kukaribia kujiunga na klabu hiyo ya Italia. (Fabrizio Romano)

West Ham wameelekeza darubini yao kwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ujerumani Niclas Fullkrug, 31, wanapomtafuta mshambuliaji mpya. (Sky Sports)

Arsenal wanavutiwa na winga wa Bayern Munich na Ujerumani Leroy Sane lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hana nafasi ya kuhama msimu huu wa joto. (Sky Germany)

Kocha wa zamani wa Newcastle Steve Bruce, 63, yuko kwenye mazungumzo ya kuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Jamaica. Muingereza huyo hajafanya kazi tangu alipofutwa kazi na West Brom Oktoba 2022. (Mail)

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button