MUNA BOLA KUISHTAKI SINGIDA BLACK STARS FIFA
Winga wa Singida Black Stars, Manu Bola 🇨🇩 ameipeleka klabu yake katika Shirikisho la soka duniani (FIFA), akishinikiza kuvunjiwa mkataba pasipo kufuata utaratibu huku akidai mishahara ya miezi mitatu nyuma (May, June na July) na bonasi kibao.
Bola anasema wakati anaondoka Lupopo na kujiunga na timu ya Ihefu (kwa sasa Singida) makunaliano ulikuwa kupelekwa Yanga baada ya msimu kumaliza hivyo alisaini mkataba wa miaka miwili na nusu. Alitarajiwa kuitumikia Yanga kwa miaka miwili iliobaki huku Singida wakiendelea kumlipa kwa mujibu wa mkataba.
“Nilikuwa nimesaini mkataba wa misimu miwili na nusu na IHEFU na sasa ikawa Singida black stars, nilicheza nusu msimu tu msimu uliopita, nilitakiwa kwenda Yanga lakini haikufanikiwa hivyo hapa nipo Dar es Salaam sifanyi mazoezi imepita mwezi mmoja viongozi wa Singida black stars hawasemi chochote na walianza mazoezi lakini hawanielezi chochote kwani walijua natakiwa kwenda Yanga.
“Tulisaini makubaliano kuwa ni Singida Black stars ndio wataendelea kunilipa na kabla ya kuondoka lazima wanipe mshahara wa mwezi May, Juni, na Julai. Bonaso yangu ya kusaini iliyobaki lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa ndio maana nimeamua kwenda kushitaki FIFA.”