Eng. Hersi Said ambae ni Rais wa Yanga SC na Makamu wake Arafat Haji wamefanikiwa kumrejesha kazini Ally Kamwe kwenye nafasi yake ya Meneja Habari na Mawasiliano na Tayari amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Klabu hiyo.
Ally Kamwe ameeleza changamoto zake kwa viongozi zilizompelekea kuchukua uamuzi wa kujiuzulu mbele ya Uongozi na kwa maslahi ya pande zote mbili wamekubaliana kuzifanyia kazi.