SINGIDA FOUNTAIN GATE YAFUNGULIWA NA KUFUNGIWA TENA
Timu ya Fountain Gate zamani Singida fountain Gate imefunguliwa kufanya usajili baada ya kumlipa aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo Shafiq Batambuze, licha ya kufunguliwa bado timu hiyo imefungiwa kusajili kwakua bado inadaiwa na wachezaji pamoja na Kocha.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini TFF leo Julai 28, imeeleza kufunguliwa na kufungiwa kwa timu hiyo.
“Shirikisho la kimataifa la Mpira wa miguu FIFA limeiondolea Fountain Gate (Singida Fountain Gate) adhabu ya kusajili wachezaji baada ya kukamilisha malipo ya aliyeluwa mchezaji wake Shafiq Batam-buze” ilieleza taarifa hiyo na kuongeza;
“Awali Shafiq Batambuze mwenyeji wa Uganda alifungua kesi FIFA dhidi ya klabu hiyo ya Ligi Kuu kwa kushindwa kumlipa malimbikizo ya mshahara na ada ya usajili”
“Hata hivyo Fountain Gate bado inaendelea kutumikia adhabu ya kufungiwa kusajili wachezaji kwani bado haijawalipa wachezaji Paschal Wawa,Bruno Gomez, na Kocha Thabo Senong ambao walishinda kesi FIFA dhidi ya Klabu hiyo” Ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa Instagram