KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amewakingia kifua washambuliaji wake akiwemo nyota mpya, Joseph Guede kuwa wanahitaji muda wa kuzoea mazingira na kuendelea kumpa muda wa kucheza kila mechi.
Amesema amekuwa akimpa nafasi nyota huyo lakini pia washambuliaji wake wengine akiamini kuwa watakuja kuwa vizuri lakini kwa sasa anahitaji mpira kuingia katika nyavu za wapinzani.
Yanga mechi ya pili wanapata ushindi kwa tabu ikiwa na Dodoma jiji kwa kushinda bao 1-0 na juzi dhidi ya Mashujaa FC kwa kuvuna alama tatu zingine kwa ushindi wa mabao 2-1, mechi zote zilichezwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar-es-Salaam.
Kocha Gamindi amesema mchezo ulikuwa mzuri licha ya wapinzani waliwapa ushindani, anamini kikubwa ni amepata alama tatu muhimu na sio nani amefunga.
Amesema kama mwamuzi angekuwa makini basi walistahili kupata penalti mbili baada ya wachezaji wake kufanyiwa madhambi ndani ya boksi, ulikuwa mpira ni mzuri kwasababu Yanga waliumiliki mchezo na kutengeneza nafasi nyingi lakini kitendo cha kukosa umakini kwenye eneo la ushambuliaji iliwagharimu.
“Tulikuwa na mchezo mzuri muda wote tulikuwa tunashambulia na mfano kipindi cha kwanza tulipata penalti mbili kwa makosa waliyofanya wapinzani lakini hatukupata hata moja, Tulicheza vizuri sana kipindi cha kwanza kwasababu niliwaambia kuwa bao moja halina tofauti kubwa ndio maana wapinzani walipata nafasi moja na kusawazisha bao na ikawa ngumu kurudi mchezoni.
Ni kweli bado safu ya ushambuliaji haijaweza kuwa imara, ukiangalia Guede amejiunga hivi karibuni anahitaji kupata muda wa kuzoea, kuhusu Kennedy Musonda alikuwa majeraha, lakini naendelea kuwapa maelekezo ninaimani watakuja kufanya vizuri .
Kwa sasa kikubwa mpira kuingia nyavuni , umeona Mudathir ameweza kufunga bao la pili na kutupatoa ushindi na kuondoka na pointi, tunarudi uwanja wa mazoezi kwa ajili ya mchezo ujao,” amesema Gamondi.
Kuhusu kuwatoa Khalid Aucho na Pacome Zouzoua, Gamondi, amesema walionekana kuumia ikabidi awapumzishe kuhofia michezo mingine ya mbele ambayo ni mingumu ukiwa wa Tanzania Prisons na Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad
“Tuna mechi ngumu tunahitaji kuwa makini , kama mchezaji anapopata majeraha na unaendelea kumuacha aendelee kuchezahata kama lilikuwa dogo basi litaongezeka zaid,” amesema Gamondi.