KITAIFA

MIKATABA MIBOVU INAVYOWATESA YANGA..ISHU YA FEISALI NA OKRAH

Baada ya Yanga SC kufungiwa na FIFA kutosajili wiki iliyopita, naona lawama nyingi zinaenda kwenye mikataba yao.

Wapo wanaodai kwamba wana mikataba mibovu hivyo eneo lao la sheria lijitathmini sana.

Kachero nimefuatilia baadhi ya kesi zao na kugundua kwamba shida wala sio mikataba yao ni mibovu kama inavyodhaniwa.

Nitakupa visa Vitatu hapa alafu mtaniambia mmegundua shida ni nini.
Kesi ya Feitoto, Okrah na Kambole.

Mkataba wa Feitoto uliandikwa kwamba, Fei akitaka kuvunja mkataba basi alipe thamani ya signing fee yake (Mil 100 kwa miaka 4, kila mwaka Mil 25) na mishahara isiwe chini ya miezi 3 (Mil 4 kila mwezi).

Ndiyo maana alilipa Mil 112, hakujipangia tu bei hivi hivi ni mkataba. Mpaka hapo kuna shida? Hakuna shida kwasababu mkataba upo sahihi sio mbovu.

Yanga SC tena, ilikubaliana na Bechem Utd ya Ghana kutoa USD 120,000 (sawa na Milioni 313,800,000 za Kitanzania) kama ada ya Uhamisho wa Okrah ambapo Yanga imeripotiwa kulipa dola 20,000 za kimarekani (Sawa na Milioni 52,300,000 za Kitanzania) ambazo walilipa ili ITC ya mchezaji ipatikane hivyo bado deni la dola za kimarekani 100,000 (Sawa na Milioni 261,500,000 za kitanzania).

Kwa Kambole walikaa mezani wakakubali kumalizana na kukubaliana kuwa Yanga SC itamlipa kambole anachodai ili wamalizane. Mkataba haukuwa mbovu mwanzoni ndiyo maana wasomi wa kambole walisaini na yeye mwenyewe.

Kumbe mikataba yao na wachezaji hawa watatu ilikuwa ipo sawa tu ndiyo maana wanasheria, wakala na wachezaji wenyewe wakaikubali na kuisaini kama hawa Wachezaji na wafanyakazi wao wengi waliopo klabuni hivi sasa walivyosaini na wanaitumikia.

Kesi zikawa Yanga SC hawataki kumuachia Feitoto licha ya kwamba mkataba umeelekeza ulivyoelekeza, kudaiwa na Bechenm United ada ya uhamisho na wameshaenda FIFA, Okrah na Kambole kwa kutowalipa malipo yaliyokubaliana walipane walipokuwa mezani.

Ishu ya Kambole imetumika kama mfano tu kwasababu kwa sasa wameshalitatua.

Credit: Abissay Stephen.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button