DJIGUI DIARRA ASAINI MKATABA MPYA YANGA
DJIGUI Diarra Asaini Mkataba Mpya Yanga, Golikipa wa Yanga na Timu ya Taifa ya Mali, Djigui Diarra ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Young Africans SC hadi 2027.
Diarra aliyesajiliwa na Yanga Agosti 2021 akitokea Stade Malien ya nchini kwao Mali Mkataba wa sasa na Yanga ulikuwa unatamatika mwisho wa msimu wa 2024/25, hivyo Kwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili unamuweka Diarra Jangwani mpaka msimu wa 2026/2027.
Ubora wa Diarra akiwa langoni kulinda nyavu zisitikiswe unajieleza kwani ndiye anashikilia Tuzo ya Kipa Bora w Ligi Kuu ya NBC kwa misimu miwili mfululizo ambayo ni 2021-2022 na 2022-2023.
Pia kipa huyo msimu wa 2023-2024 alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika wa Mali baada ya kuonekana kuwa bora zaidi kuwazidi wenzake wanaocheza ndani ya Bara la Afrika kutokea nchini Mali.
Mbali na hilo, Diarra alimaliza Ligi Kuu ya NBC akiwa na clean sheet 14 na kuifanya Yanga kuwa kinara wa timu zilizoruhusu magoli machache zaidi msimu wa 2023-2024 na kubeba Ubingwa.
Diarra amekuwa sehemu ya mafanikio ya Young Africans tangu alipojiunga nao ambapo msimu wa 2022-2023 aliifikisha Timu hiyo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku 2023-2024 wakicheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tayari Diarra amecheza Young Africans kwa misimu mitatu na yote hiyo wameshinda Ubingwa wa Ligi Kuu ya
NBC mfululizo sambamba na Kombe la CRDB Bank Federation.