KITAIFA

MAYELE AIPANIA MECHI NA TAIFA STARS

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya DR Congo, Fiston Mayele amesema katika mechi yao ijao dhidi ya Tanzania watacheza kama fainali kwani wanataka kuitumia mechi hiyo ili wafuzu hatua ya mtoano

“Mechi na Taifa Stars tutacheza kama fainali kwasababu sisi tunatak ushindi ili tufuzu hatua inayofuata. Utakuwa ni mchezo mzuri sana ila watanzania wajiandae” amesema Mayele

Mchezo wa kumaliza katika kundi F ambalo yupo Taifa Stars na DR Congo unapigwa tarehe 24 majira ya saa tano usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo katika msimamo wa kundi F ni Morocco ndio anaongoza akiwa na Point 4, akifuatiwa na DR Congo na Zambia wenye point 2, Huku kundi likishikwa mkia na Taifa Stars wenye Point 1.

Ukitazama katika kundi Kama Stars akipata ushindi mbele ya DR Congo anajiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya robo fainali ambapo kama Stars ikifanikiwa itakuwa ni historia nzuri kuwekwa na nchi ya Tanzania.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button