KITAIFA

BREAKING NEWS: BARBARA ARUDI SIMBA…MO HATAKI MASIHARA

HABARI za Simba Leo ni za moto, za hivi punde tulizozinyaka ni kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez amekubali kurudi ndani ya klabu hiyo.

Makubaliano baina ya pande zote mbili, yaani Bodi ya Wakurungenzi na upande wa Barbara yameafikiwa siku ya jana na kwa sasa kinachosubiriwa ni kutangazwa kwake kama kiongozi mpya klabu hapo.

Uongozi wa Simba upo kwenye mabadiliko ya ndani ambapo nafasi zinazohusishwa sana, ni nafasi ya CEO Iman Kajula ambaye amekubali kujiuzulu kwenye nafasi hiyo, pamoja na nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungenzi inayokaliwa na Salim Try Again.

Kuna mabadiliko kadhaa ambayo tayari yamefanyika ndani ya Simba, tena kwa siri kubwa ambapo Crescentius Magori na Swedy Nkwambi wamerudishwa na kupewa nafasi ya kusimamia kamati ya usajili wa timu hiyo.

Soka la Bongo linaelewa kwamba hapo awali, Barbara aligoma kurudi Simba mpaka pale baadhi ya watu aliowataja kuwa hahitaji kufanya nao kazi, watakapoondoka ndiyo atarudi.

Kwa habari hizi ina maanisha kwamba, Barbara Gonzalez alichokitaka kimetimizwa na yupo huru kufanya kazi ndani ya miamba hiyo ya soka Tanzania na Afrika.

Enzi za utawala wake kabla hajatangaza kuachia kiti chake cha Ukurugenzi, Barbara Gonzalez alifanikiwa kwa kiasi chake kuipambania Simba ndani na nje ya Tanzania.

Mafanikio yake yalikuwa ni kutetea ubingwa wao kwa msimu wa 2020/21, Kuchukua kombe la Shirikisho na kufanya sajili bora kulinganisha na miaka ambayo yeye aliondoka.

Moja ya sababu iliyomuondoa Simba kipindi hicho, inaelezwa ni fitina za baadhi ya Viongozi na watu aliokuwa anafanya nao kazi, kitu kilichomfanya kushindwa kuvumilia na kujiuzulu nafasi yake.

Kama ambavyo Soka La Bongo tuliripoti habari za Simba ya kwamba, wanafanya mambo yao kimya kimya na Afisa Habari wa Klabu hiyo Ahmed Ally alisema kila kitu kinafanyika kwa umakini na ustadi mkubwa, ikiwemo usajili wa msimu wa dirisha hili.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button