KITAIFA

MO DEWJI MWISHOWE ATACHOKA SIMBA

Kuna vitu vingine vinaumiza sana. Ni kama hili la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Klabu ya Simba. Limekaa muda mrefu na sasa linatia kizunguzungu. Mchakato ulianza vizuri miaka saba nyuma. Alianza bilionea Mohamed Dewji kwa kuitisha mkutano na wanahabari kisha kuweka nia yake ya kuwekeza ndani ya Simba.

Kwa wakati ule Dewji alisema wazi anahitaji kununua asilimia 51 ya hisa za klabu ya Simba kwa kiasi cha Shilingi 20 bilioni. Ni fedha nyingi hata kwa kuzitamka tu. Zilikuwa fedha nyingi zaidi kwa wakati ule. Wakati Dewji anataka kuwekeza Simba, bajeti yao kwa mwaka haikuwa inafika Shilingi 2 bilioni. Simba ilikuwa katika umasikini mkubwa. Maisha yao yalikuwa ya kuunga unga.

Simba haikumudu kusafiri kwenda mikoani kwa usafiri wa ndege. Walizurura na basi kama vile kampuni ya usafirishaji. Iliumiza sana. Simba ingekwenda Songea kwa basi. Sio basi tu sema Coaster kwa masafa marefu kama hayo! Ingekwenda Bukoba na Mwanza kwa basi. Ilikuwa ni umasikini mkubwa. Simba ilikuwa ikisajili wachezaji wa bei nafuu. Haikuweza kushindana sokoni na Yanga ya Yusuf Manji au Azam FC. Ilikuwa na hali mbaya sana. Ilikuwa ni jambo la kawaida kusikia wachezaji wa Simba wamekaa miezi kadhaa hawajalipwa mishahara.

Wakati huo Simba ilikaa miaka mitano bila kutwaa taji la Ligi Kuu. Kuna misimu kadhaa ilimaliza katika nafasi ya tatu na ya nne. Haikuwa na ushindani tena. Iliumiza sana kwa mashabiki. Ndio nyakati hizi Dewji alijitokeza na kusema anataka kununua asilimia 51 ya hisa kwa Shilingi 20 bilioni. Nani angekataa? Hakuna. Ilikuwa ni kama Nabii ameshuka kuja kuokoa kizazi kinachoteseka sana … Inaendelea

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button