KITAIFA
SIMBA QUEENS AENDELEZA UBABE MBELE YA YANGA
KATIKA Ligi ya Wanawake Simba Queens imepeta mbele ya Yanga Pricess kwenye Kariakoo Dabi ya Wanawake mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Baada ya dakika 90 ubao umesoma Yanga Princess 1-3 Simba Queens ambapo pointi tatu zimeelekea kwa Simba Queens.
Dakika 45 za mwanzo hakukuwa na mbabe kwa timu zote ambapo ubao ulikuwa unasoma 0-0 mambo yalibadilika kipindi cha pili kwa Simba kupata mabao.
Ni Aisha Mnunka huyu alitupia mabao mawili dakika ya 49 na 90 na bao moja ni mali ya Jentrix Shikangwa ilikuwa dakika ya 66.
Bao la kufutia machozi kwa Yanga limefungwa na Kaeda Wilson dakika ya 90.