Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney na wanaamini kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ataleta uzoefu na uongozi kwenye kikosi chao (90min)
Hata hivyo, Tottenham wanaweza kumnunua Toney iwapo kutakuwa na ushindani wa kutosha kuipata sahihi yake na kutoa pauni milioni 45. (GivemeSport)
Manchester United inalenga kuwaachilia wachezaji 12 msimu huu wa joto, akiwemo fowadi wa Uingereza Marcus Rashford, 26, na kiungo wa kati wa Brazil Casemiro, 32. (Mirror).
Mustakabali wa Mauricio Pochettino kama meneja wa Chelsea upo katika mizani na unaweza kutegemea iwapo anaweza kufuzu kwa shindano la Uropa kwa msimu ujao(Times)
Mshambulizi wa Napoli Victor Osimhen, 25, anakaribia kujiunga na Paris Saint-Germain , lakini mshambuliaji huyo wa Nigeria pia ameivutia Chelsea . (Il Mattino – kwa Kiitaliano)
Newcastle United wanaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 20 Ousmane Diomande, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro 80m (£68.7m). (A Bola – kwa Kireno)
Tottenham wako katika nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, kutoka Chelsea msimu huu – licha ya kumezewa mate na Newcastle. (Football Insider)
Arsenal wanahusishwa na kutaka kumnunua beki wa kushoto wa Real Madrid Ferland Mendy, 28, huku Liverpool, Manchester United na Newcastle pia wakimtaka Mfaransa huyo. (L’Equipe – kwa Kifaransa)
Meneja wa Aston Villa Unai Emery anashinikiza klabu hiyo kumsajili winga wa Athletic Bilbao mwenye umri wa miaka 21 Nico Williams.(GiveMeSport)
Villa wanamfuatilia kwa karibu winga wa Leeds United Mholanzi Crysencio Summerville, 22. (Football Insider)
Tottenham inaweza kuipa Genoa fursa ya kumsajili kwa mkopo beki wao Mwingereza Djed Spence, 23, kwa mkataba wa kudumu ili kubadilishana na mshambuliaji wa Iceland Albert Gudmundsson, 26. (Calcio Mercato – kwa Kiitaliano).
Arsenal wako tayari kukubali ofa za pauni milioni 20-25 kwa kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey, 30, na bado wanavutiwa na kiungo wa kati wa Aston Villa wa Brazil Douglas Luiz, 25, kama mbadala wake. (Football Insider)
Feyenoord wamemtambua mkufunzi wa FC Twente Joseph Oosting kama mmoja wa walengwa wao wakuu wa ukocha, iwapo watampoteza Arne Slot kwa Liverpool (Mirror)
West Ham wamekuwa kwenye mazungumzo na meneja wa zamani wa Uhispania Julen Lopetegui “kwa miezi”, na mkataba wa bosi wa sasa David Moyes unamalizika Juni. (Mundo Deportivo – kwa Kihispania)
Newcastle wanatazamiwa kumsaini beki wa Uingereza wa kikosi cha Chini ya miaka 21 Lewis Hall, 19, kwa mkataba wa kudumu msimu wa joto. (Football Insider)
Erik ten Hag atakabiliwa na kupunguzwa kwa mshaharawake kwa 25% kama meneja wa Manchester United ikiwa ataendelea kuwa meneja huku klabu hiyo ikitarajiwa kukosa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa. (ESPN)